Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, June 21, 2016

CHUO KIKUU TEKU CHAJIPANGA KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA KUONGEZA WASOMI

 
Wahitimu wa fani mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo kikuu cha TEKU baada ya kumalizika kwa Mahafali ya 9 yaliyofanyika juzi chuoni hapo

Baadhi ya Wazazi jamaa na marafiki waliojumuika pamoja na Wahitimu wa Diploma ya Habari na mawasiliano kwa umma wakiwa katika picha ya pamoja

Wahitimu wakiwa ukumbini wakifuatilia kwa makini matukio yanayoendelea

Baadhi ya Wahitimu wa Fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya uuma wakiwa katika picha ya pamoja

Wahitimu wa Fani ya Uandishi wa habari wakifurahia jambo baada ya kumaliza sherehe za mahafali, Wa kwanza kulia ni Godfrey Kahango kutoka gazeti la Mwananchi Mbeya.

Baadhi ya Ndugu wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu Godfrey Kahango na Rogate Andrew

Godfrey Kahango akiwa katika pozi

Godfrey Kahango akifurahia kulishwa keki na dada zake akiwemo Amina Said kutoka Star Tv Mbeya (Kulia)

Godfrey Kahango akilishwa keki na Venance Matinya ikiwa ni Ishara ya kumpongeza kwa kumaliza masomo yake ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma katika ngazi ya Diploma
ILI   kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na wahitimu wa fanimbali mbali nchini, Uongozi wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo jijini Mbeya umejipanga kuhakikisha unaongeza kozi chuoni hapo.
 
Akitoa taarifa ya kurugenzi ya Elimu Anuai ya Chuo Kikuu cha TEKU, Kaimu Mkurugenzi, Simwaba Joseph alisema chuo kinatarajia kuongeza programu za uuguzi, ualimu wa Sekondari na Msingi kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017  ili kusaidia vijana wengi kujinasua kutoka katika wimbi la ukosefu wa ajira.
 
Kaimu Mkurugenzi huyo alitoa taarifa hiyo juzi katika sherehe za Mahafali ya Tisa ya Chuo hicho zilizofanyika katika Ukumbi wa mikutano uliopo Block T jijini Mbeya ambapo wahitimu walitunukiwa Shahada katika fani mbali mbali ikiwemo Uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma.
 
Joseph alisema katika Mahafali hayo jumla ya wanafunzi 191 waliajiandikisha lakini hadi wanahitimu ni  wanafunzi 157 watapewa shahada kutokana na fani walizosoma, na wanafunzi 34 hawajaweza kuhitimu mafunzo yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za wengine kushindwa kulipa ada.
 
Awali Akisoma risala ya wahitimu hao, Lwiza John, aliyesoma fani ya Uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma aliuomba uongozi wa chuo hicho kupunguza kiwango cha ada kwa kuwa imekuwa ni mzigo kwao.
 
"Kiwango cha ada ni kikwazo kwetu na tunaomba uongozi ulifikirie hili ili ada kwa mwanafunzi wa astashahada ipungue kutoka Sh700,000 hadi 600,000 na stashahada ipungue kutoka 900,000 hadi 800,000," alisema Lwiza.
 
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Tully Kasimoto aliiomba Serikali kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwa shule na vyuo  binafsi,hali ambayo wamedai kuwa inadumaza utendaji kazi wao kwa kushindwa kuboresha huduma hiyo muhimu kwa jamii.
 
Alisema vyuo binafsi vinatozwa kodi nyingi tofauti na vyuo vya serikali hali inayowapa wakati mgumu wamiliki hao na kupelekea wanafunzi kulalamikia ukubwa wa ada pasipokujua kuwa sababu ni mlundikano wa kodi.
 
Alisema lengo la wamiliki wa vyuo na shule binafsi ni kutoa huduma kwa vijana na siyo kufanya biashara na kwamba wanashindwa kuboresha mazingira ya elimu kwa vijana kutokana na fedha nyingi kutumika katika ulipaji wa kodi.
 
"Suala la kodi ni changamoto kwetu kwani tunatoa kodi nyingi tofauti na vyuo vya serikali na hili linadumaza utendaji kazi wetu kutokana na sisi tuna lengo la kutoa huduma kwa vijana na siyo kwamba tunafanya biashara, "alisema Kasmoto.
 
Kuhusu udahili wa wanafunzi wasiokuwa na sifa ya kujiunga na vyuo, Kasmoto alisema suala hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani wanaodahili wanafunzi hao wamekosa uaminifu na hawana nia nzuri ya kukomboa vijana.
 
"Hivi sasa serikali ndiyo inasimamia suala hilo la udahili wa mfumo wa pamoja na ili kuhakikisha vyuo havidahili wanafunzi hewa ni vyema mfumo uchunguzwe upya na hata hivyo mwanafunzi huyu kwa vyovyote vile atashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yake, "alisema.
 

No comments: