Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, January 18, 2015

SHEREHE ZA KUAGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2015 ZA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA MBEYA ZAFANA, WATUMISHI WAPEWA ANGALIZO KUONGEZA BIDII.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa meza kuu pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka yaMaji safi na usafi wa Mazingira Mbeya(Mbeya Uwsa).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akiwaongoza watumishi wa mamlaka ya maji Mbeya kuimba wimbo wa Solidarity.

Kaimu Mkurugenzi wa Mbeya Uwsa, Mhandisi Kimambo akitoa utambulisho katika sherehe za kuaga na kuukaribisha mwaka 2015.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mbeya Uwsa, Jaji Atuganile Ngwala akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.


Venance Hawera akisoma risala ya wafanyakazi wa mamlaka mbele ya mgeni rasmi.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,akitoa hotuba kwa wateja wa mamlaka pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akipokea tuzo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya baada ya Mamlaka kutambua mchango wa jeshi hilo katika mafanikio yao


Mwakilishi wa Chama cha Waandhishi wa habari Mkoa wa Mbeya(mbeya press club) Venance Matinya, akipokea tuzo kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya baada ya Mamlaka ya maji kutambua mchango wa wanahabari katika mafanikio ya mamlaka hiyo.


Mshehereshaji wa sherehe hiyo, Amir Sapi akiendelea kuendesha ratiba ya sherehe.
Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya Maji, Jaji Atuganile Ngwala, akitoa shukrani za kabila la wanyakyusa katika sherehe za mamlaka hiyo.


Mwenyekiti wa bodi akiwaongoza wateja na watumishi kucheza muziki.


Mwenyekiti wa Bodi akitoa zawadi kwa niaba ya mamlaka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.


Wafanyakazi wa mamlaka ya maji mbeya wakitoa zawadi kwa wastaafu wa mamlaka hiyo.


Wafanyakazi wakijimwayamwaya kwa burudani ya muziki.


Vikundi vya sanaa vikitoa burudani katika sherehe hizo.




 Baadhi ya madiwani waliohudhuria sherehe hizo.


Wageni mbali mbali na watumishi wakionekana wakiwa ukumbini.



Katibu wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo, Neema Stantoni, akiwa pamoja na mmoja wa wafanyakazi wa mamlaka katika sherehe hizo.


MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya(Mbeya Uwsa) imesema inajivunia mafanikio ya kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa utendaji wa Mamlaka za maji Kitaifa na nafasi ya pili kwa utekelezaji wa shughuli za Maji taka na usafi wa mazingira.



Hayo yalibainishwa na Wafanyakazi wa Mbeya Uwsa katika risala yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe  ya kuuaga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka 2015 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini hapa.



Walisema matokeo hayo yametokana na tahmini iliyofanywa na EWURA katika kupima utendaji kazi wa Mamlaka zote kitaifa kwa mwaka uliopita hivyo kuonesha Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya kushika nafasi ya pili kwa utendaji wa jumla na nafasi ya pili kwa usafi wa mazingira.



Walisema matokeo ya tathmini hiyo yanatoa hamasa ya kufanya vizuri katika mwaka 2015 na lengo likiwa ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya jumla na utekelezaji wa shughuli za mazingira.



Waliongeza kuwa Silaha kubwa ya mafanikio hayo ni mpango uliopo wa matokeo makubwa sasa(BRN) ulioanza Juni 2014 hadi Julai 2018 ambapo Mamlaka hiyo imepata mafanikio katika utekelezaji wa mambo mbali mbali kwa mwaka 2014 ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2001 ilipokuwa ikianzishwa.



Waliyataja mafanikio hayo kuwa ni ongezeko la wateja wa maji safi kutoka 9168 mwaka 2001/2002 hadi wateja 40709 mwaka 2014/2015, urefu wa mabomba ya kusafirisha na kusambazia maji kutoka kilomita 108 hadi 710, wateja wa mati taka kutoka 42 hadi 1466 na jumla ya dira zilizofungwa kutoka 1931 hadi 40709.



Waliongeza kuwa uwiano wa wateja wenye dira umeongezeka kutoka asilimia 21.06 hadi asilimia 98.5, kupungua kwa upotevu wa maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia 30.2, kuongezeka kwa uwezo wa kuzalisha maji kwa siku kutoka 18700 mita za ujazo hadi mita za ujazo 51000, kiwango cha huduma kutoka asilimia 69 hadi asilimia 95 na kuongezeka kwa muda wa upatikanaji wa maji kutoka masaa 14 hadi masaa 23.1.



Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa bodi ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Jaji Atuganile Ngwala, alisema mafanikio yaliyopatikana mwaka 2014 yametokana na ushirikiano baina ya uongozi wa bodi na watumishi wa mamlaka na wateja wao.



Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alitoa wito kwa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuacha kubweteka na mafaniko waliyoyapata bali kuongeza kasi ya kuzikabili changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho.



Aliwataka wafanyakazi kuacha kuishi maisha ya juu hali itakayosababisha kuwa na tama na kuwapelekea kutukuwa waaminifu katika mali za mamlaka na kuwasihi kuishi maisha kulingana na uwezo na vipato vyao.



Aliongeza kuwa timu za ukaguzi za Mamlaka hiyo hasipaswi kukaa ofisini bali zizunguke jambo litakalosaidia kupatikana kwa mtandao wa watu wanaojiunganishia maji, wezi wa maji na wanaoiba Dira za maji.



Kandoro alisema ni jukumu la kila mwananchi kushirikiana katika utunzaji wa mazingira, kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuacha tabia ya kulima , kuchunga mifugo, kuchoma moto kwenye vyanzo vya maji hali itakayochangia uharibifu wa mazingira na kukauka kwa vyanzo vya maji.



Alisema takwimu zinaonesha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita jumla ya vyanzo vya maji 40 vimekauka kutokana na kuharibu mazingira na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji bila kuchukua tahadhari zozote.



Mwisho.
Na Mbeya yetu


No comments: