Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, December 2, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA BARABARA YA NELSON MANDELA TEMEKE JIJINI DAR LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya Ufunguzi wa jiwe la Msingi la Barabara, wakati wa ufunguzi wa Barabara hiyo ya Mandela uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya Enrico Strampeli, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Nelson Mandela, iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Desemba 2, Temeke jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli , wakikata upete kwa pamoja ikiwa ni ishala ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela, uliofanyika leo Desemba 2, Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na (kulia) kwa Balozi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, baada ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Nelson Mandela uliofanyika leo Desemba 2, Temeke jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya, Enrico Strampeli, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliowezesha ujenzi wa Barabara hiyo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: